Mkali Kwanza Mark ‘Makamua’ Paul ameiambia Bongo5 ‘exclusively’ kuwa iwapo mambo yakienda kama anavyotarajia hivi karibuni atawaacha mdomo wazi mashabiki wa muziki wa Tanzania kwa kumshirikisha bosi wa Konvict Music, Akon.
“Sijakiongelea kwanza kwasababu nataka kifike kwenye climax halafu niweze kuongea,” amesema Makamua kujibu swali la kwanini suala hilo amechelewa kulisema.
“Maongezi yameshafanyika na kila kitu kimeshafanyika, actually tulikuwa tunajaribu kutuma kitu fulani kwake ili afanye kitu then zirudi halafu na mastering tujue tunafanya nini, tunabalance vipi huku na kwao halafu tujue project inaraniwa vipi.”
Akon
Makamua amesema wimbo huo unaitwa Bado Kujuana. “Yaani bado kujuana
you need my money fine you can chop my money but first me I want to get
to know you better before you chop my money. Nimeimba Kiswahili na
Kiingereza lakini Kiingereza kimetawala zaidi.”Akiongea jinsi alivyoweza kupata connection na Akon Makamua amesema, sana sana online na vitu kama hivyo, si unajua tena wenzetu wamepata nafasi ya kukutana na watu kama hao. Kwahiyo sana sana South Africa pale kuna jamaa yuko close na jamaa.”
Source | Bongo5
No comments:
Post a Comment